1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Waislamu wasali Ijumaa ya mwisho ya Ramadhani.

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0k

Mamia kwa maelfu ya Waislamu wamesali katika msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem katika Ijumaa ya mwisho katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan huku kukiwa na ulinzi mkali wa polisi wa Israel kuzuwia kutokea machafuko.

Katika hotba yake, Imam Yussef Abu sneineh amewataka wapalestina kuungana na kujilinda dhidi ya kurejea tena katika mizozo baina ya chama cha rais Mahmoud Abbas cha Fatah na chama tawala cha Hamas.

Akishutumu Israel kuikalia nchi yao na mbinyo wa kimataifa , amesema kuwa Wapalestina wanakabiliwa na njama mbaya dhidi yao na ardhi yao.

Wakati huo huo makao makuu ya kiongozi wa kanisa Katoliki, Vatican , yamesema leo kuwa mdahalo unaoendelea na dini ya Kiislamu ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine, kutokana na hotuba ya utata ya Pope Benedict 16 nchini Ujerumani ambayo imezusha maandamano kwa Waislamu duniani.

Hali tunayojikuta inaonyesha wazi kuwa , licha ya njia ya mdahalo wa kweli kuwa ngumu wakati mwingine, lakini ni muhimu kuliko wakati mwingine hivi sasa, amesema kadinali Paul Poupard katika salam zake kwa Waislamu katika kumaliza mfungo wa Ramadhan.

Poupard ambaye anaongoza baraza la makadinali linalohusiana na mdahalo na dini mbali mbali, amechukua hatua hiyo kwa kutoka katika vyombo vya habari kile ambacho sasa kinaonekana kuwa jambo la kawaida , salamu kwa viongozi wa dini ya Kiislamu.