1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem: Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Rice, anakutana na waziri mkuu wa Israel na rais wa Wapalastina

18 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQv

Muda mfupi kabla ya kufanyika mkutano wa kilele juu ya Mashariki ya Kati mjini Jerusalem, Israel na Marekani zimezidisha mbinyo kwa Wapalastina. Waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, na Rais George Bush wa Marekani walikubaliana katika mazungumzo ya simu kwamba waisusie pia serekali ijayo ya Wapalastina ikiwa serekali hiyo haitaitambua wazi wazi dola ya Israel na pia kuwachana na matumizi ya nguvu. Katika kuutayarisha mkutano huo wa kilele, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, alikutana mjini Ramallah na rais wa Wapalastina, Mahmud Abbas. Hii leo Bibi Rice pia atakutana na Bawana Olmert. Kesho wote watatu watakuwa na mazungumzo ya pamoja kuangalia uwezekano wa kuufufua tena mwenendo wa amani wa Mashariki ya Kati.