1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Olmert na Livni kushirikiana kikazi

6 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4L

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema hatomfuta kazi waziri wake wa mambo ya nje Tzipi Livni licha ya waziri huyo kumtaka hadharani bwana Olmert ajiuzulu.

Livni alitoa tamko hilo wiki iliyopita kufuatia kutolewa kwa ripoti rasmi iliyomkosoa waziri mkuu olmert kwa jinsi alivyoendesha vita vya Lebanon.

Haya yamejitokeza baada ya waziri mkuu Olmert na waziri wake Tzipi Livni kukutana kwa muda mfupi baada ya kumalizika kikao cha baraza la mawaziri cha kila mwisho wa wiki ambacho kimejadili zaidi masuala ya kidiplomasia.

Bwana Olmert amefanikiwa kuituliza miito ya kumtaka ajiuzulu iliyokuwa inatolewa na pande mbali mbali za kisiasa nchini Israel.

Hata hivyo tume iliyochaguliwa na serikali kuchunguza juu ya vita vya Lebanon itatoa ripoti ya mwisho katika muda wa miezi kadhaa ijayo na huenda ikapendekeza waziri mkuu Olmert aondoke madarakani.