1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Wahanga wa mauaji ya kifashisti walalamikia ruzuku

6 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbl

Mamia ya wahanga wa mauaji ya kifashisti wamekusanyika nje ya afisi za serikali mjini Jerusalem nchini Israel kupinga kile wanachokitaja kuwa ni dharau kubwa kutoka kwa serikali yao.

Waandamanaji hao wanapinga matamshi ya ofisi ya waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ya wiki iliyopita kwamba kuanzia mwaka 2008 serikali itawalipa ruzuku ya euro 15 kwa mwezi wahanga wa mauaji ya kifashisti walio hai na ambao wana umri wa zaidi ya miaka 70 wanaoishi nchini Israel.

Mashirika yanayowatetea wahanga hao yemepinga malipo hayo na kusema kuwa kiwango hicho hakifai kabisa.

Wengi kati ya wahanga laki mbili na elfu hamsini wanaoishi nchini Israel wanaishi katika hali duni na wanakabiliwa na umasikini mkubwa.

Serikali ya Israel imesema kuwa itatafuta suluhisho.