1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi huru la Syria FSA, lapoteza kamanda wake leo

Admin.WagnerD12 Julai 2013

Kundi la Al-Qaeda nchini Syria leo limemuuwa kiongozi wa waasi wa jeshi huru la Syria FSA, Kamal Hamami na wapiganaji wengine wawili, katika mapigano yaliojiri katika wilaya ya pwani ya Latakia nchini Syria.

https://p.dw.com/p/1970p
waasi
waasiPicha: Reuters

Mapigano hayo yamezusha wasiwasi kati ya jeshi huru la Syria , wafuasi wake na makundi ambayo yana mafungamno na mtandao wa Al-Qaeda ambayo kwa kiasi kikubwa unawahusisha wapiganaji wasiokuwa wasyria.

Waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria wamsema kuwa Kamanda Kamal Hamami anayefahamika kwa jina maarufu la Abu Bassir al-Jeblawi, alipigwa risasi na kundi linalopigania taifa la kiislamu nchini Iraq na Syria ISIS, moja ya makundi yanayopigana vita vya jihadi nchini humo

Kamanda huyo wa waasi alipigwa risasi wakati wapiganaji wa kundi hilo la ISIS wakijaribu kuharibu kituo cha ukaguzi cha jeshi huru la Syria FSA katika mkoa wa Jabal al-Turkman kasikazini mwa wilaya ya Latakia

Kwa mujibu wa wachunguzi ambao wanategemea kwa upana taarifa kutoka mtandao wa wanaharakati, madaktari na wanasheria, wamesema waasi wa Jeshi Huru la Syria FSA walipiga risasi hewani na baada ya hapo wapiganaji wa kundi la ISIS wakajibu mashambulizi yalimuuwa Abu Bassir na kujeruhi wengie wawili wa kundi lake.

Jana kundi hilo la Kiislamu lilimuachia kiongozi mwengine wa waasi baada ya kumshikilia kwa siku 25 sambamba na waasi wengine tisa. Juma lillilopita wapiganaji kadhaa wa FSA waliuawa katika mapigano dhidi ya kundi la ISIS katika jimbo la Idlib Kaskazini Magharibi

Hata hivyo wapiganaji wa kundi la ISIS wanatuhumiwa kwa kuwawake kizuizini mateka kadhaa katika mji wa Raqa, mji mkuu pekee wa jimbo hilo ambao upo nje ya udhibiti wa utawala wa Rais Bashar al-Assad.

Wanaharakati wanaompinga Rais Assad wanaoishi katika maeneo ya waasi hivi sasa wanabadili mitazamo yao kwa kufanya kampeni dhidi ya wapiganaji wa kundi la kiislamu lenye mafungamano na Al Qaeda kutokana na ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu unaofanywa na kundi hilo.

Kwa sasa kuna makundi mawili nchini Syria yenye mafungamano Al-Qaeda yote yakiwa na asili ya Iraq, kundi la Al-Nusra ambalo linajitegemea katika harakati zake zake na ISIS .

Wakati huo huo Upinzani nchini Syria umeilaumu kamati ya Bunge la Marekani kwa kupinga mpango wa kuwapa silaha waasi nchini syria, ikihofia kwamba huenada silaha hizo zikaangukia mikononi mwa makundi ya kiislamu ya siasa kali.Mnamo siku ya Alhamisi upinzani nchini Syria ulitoa wito mwengine wa kupatiwa silaha, ukiahidi kwamba silaha hizo hazitaingia mikononi mwa makundi ya Kiislamu.

Mwandishi:Hashimu Gulana/AFP/RTRE

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman