1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Jeshi la Israel lakabiliana na kundi la wanamgambo la Hamas

Tatu Karema
12 Mei 2024

Wanajeshi wa Israel wanakabiliana na wanamgambo wa kundi la Hamas leo katika ukanda wa Gaza ikiwa ni pamoja na sehemu za eneo la kaskazini lililoharibiwa

https://p.dw.com/p/4fl0C
Eneo la Khan Yunis, Gaza, lililoharibiwa na mashambulizi ya Israel huku wakazi wakijaribu kurejelea maisha yao ya kawaida chini ya mazingira magumu.
Eneo la Khan Yunis, Gaza, lililoharibiwa na mashambulizi ya IsraelPicha: picture alliance / Ali Jadallah / Anadolu

Wapalestina wameripoti kuhusu mashambulizi makali ya Israel ya usiku kucha katika kambi ya wakimbizi ya Jabaliya na maeneo mengine ya kaskazini mwa ukanda huo ambapo maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema yanakumbwa na njaa kubwa.

Idara ya Ulinzi ya Palestina yashindwa kutoa msaada

Idara ya Ulinzi wa Raia wa Palestina, imesema haikuweza kujibu maombi mengi ya msaada kutoka pande zote pamoja naRafah,mji wa kusini mwa Gaza.

Soma pia:Israel yashambulia Gaza na kuamuru watu zaidi kuondoka Rafah

Wanajeshi wa Israel wamekuwa wakipambana na wanamgambo wa Hamas katika eneo hilo tangu jeshi lilipoteka kivuko cha eneo hilo kinachopakana na Misri wiki iliyopita.

Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari, amesema kuwa vikosi vyake vinapambana katika maeneo yote ya Gaza na kwamba mbali na Jabaliya na Zeitoun, vikosi hivyo pia vinafanya operesheni katika miji ya Beit Lahiya na Beit Hanoun, karibu na mpaka wa kaskazini na Israel.