1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Pakistan lawaua wanamgambo wawili wa Taliban

3 Februari 2023

Jeshi la Pakistan limevamia maficho ya wanamgambo katika ngome ya zamani ya kundi laTaliban la Pakistan.

https://p.dw.com/p/4N3ZP
Pakistan Peshawar Explosion der Polizeilinie
Picha: Faridullah Khan/DW

Msako huo umefanyika karibu na mpaka na Afghanistan Ijumaa, na kusababisha majibizano ya risasi ambapo waasi wawili wameuawa.

Waziri mkuu wa Pakistan Shahbaz Sharif amemuita kiongozi wa upinzani nchini humo kujibu juu ya kuongezeka kwa matukio ya vurugu, ikiwa ni pamoja na tukio ma mlipuko wa bomu lililotokea msikitini na kusababisha vivyo vya watu wapatao 101.

Jeshi limeongeza kuwa wamegundua shehena ya silaha katika maficho ya wanamgambo huko Kaskazini mwa Waziristan, katika mkoa wa Pakhtunkhwa.

Taliban wa Pakistani ni kundi tofauti lakini ni washirika wa Taliban wa Afghanistan, walionyakua mamlaka nchini Afghanistan mwaka mmoja uliopita wakati ambapo Marekani na wanajeshi wa NATO walikuwa katika hatua za mwisho za kujiondoa.