1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Umoja wa Mataifa kupiga kura kupeleka wanajeshi Haiti

Amina Mjahid
2 Oktoba 2023

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura leo Jumatatu, kuidhinisha kupelekwa kwa wanajeshi wa kigeni nchini Haiti.

https://p.dw.com/p/4X3M8
Mmoja ya raia walioandamana katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince akiwa amebeba panga kama alama ya kujilinda dhidi ya makundi pinzani ya uhalifu
Mmoja ya raia walioandamana katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince akiwa amebeba panga kama alama ya kujilinda dhidi ya makundi pinzani ya uhalifu Picha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kuidhinisha wanajeshi hao kutumia nguvu kupambana na magenge yanayosababisha machafuko katika mji wa Port-au-Prince.

Azimio lililoandaliwa na Marekani na kuonekana na shirika la habari la Reuters limetanua vikwazo vilivyowekwa na taifa hilo vinavyotumika tu kwa watu binafsi, kwamba sasa vitawajumuisha pia magenge yote nchini Haiti, jambo ambalo China ilikuwa inaliunga mkono.

Kulingana na maafisa wa Haiti, silaha zinazotumiwa na magenge nchini humo zinaaminika kutolewa Marekani.

Mwaka mmoja uliopita Haiti iliomba msaada wa Kimataifa wa kupambana na magenge hayo. Hata hivyo haijawa wazi iwapo China na Urusi zilizo na kuru ya turufu pamoja na Marekani, Ufaransa na Uingereza watakavyolipigia kura azimio hilo la Umoja wa Mataifa kuhusu Haiti.