1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi lazima uasi Madagascar

Abdu Said Mtullya22 Novemba 2010

Jeshi ambalo ni tiifu kwa uongozi wa serikali ya Andry Rajoelina limefanikiwa kuzima uasi uliofanywa na maafisa wa ngazi za chini katika kisiwa hiki cha Bahari ya Hindi

https://p.dw.com/p/QEdq
Watu wa Madagascar kwa mara nyingine wameshtushwa na uasi wa wanajeshi!Picha: AP

Waziri Mkuu wa Madagascar, Camille Vital, amesema kuwa jaribio la kuiangusha serikali limezimwa bila ya damu kumwagika, baada ya maafisa 16 wa kijeshi waliohusika na uasi huo wamejisalimisha.

Hapo awali waasi walitangaza kuwa walikuwa wanatwaa mamlaka kutoka kwa kiongozi wa sasa, Andry Rajoelina, ambaye mwaka jana pia alitwaa uongozi kutokana na kuungwa mkono na wanajeshi. Mamia ya Wanajeshi watiifu walionekana wakikusanyika karibu na uwanja wa ndege ambapo waasi walikuwa wameweka kambi yao. Maafisa waasi walikuwa wametangaza kuvunjwa idara zote za uongozi za Madagascar na kusema kuwa wameunda baraza la uongozi la kijeshi.

Waziri Mkuu Vital amesema licha ya kusikika milio ya silaha, hakuna mtu hata mmoja aliyejeruhiwa, na kwamba sasa hali imerejea kuwa shwari katika nchi hiyo.