1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG: Waziri wa zamani ahukumiwa kifungo cha nje

17 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYL

Waziri wa zamani wa sheria na utengamano wa Afrika Kusini, Adriaan Vlok, na washukiwa wengine wanne wamehukumiwa kifungo cha nje kwa kuwa na njama ya kumuua mtetezi aliyepinga ubaguzi wa rangi.

Vlok na wenzake walikiri walifanya njama ya kutaka kumuua kwa kumtilia sumu mchungaji wa kanisa, Reverend Frank Chikane. Vlok, kamanda wake wa polisi na maafisa wengine wa polisi walishtakiwa kwa kujaribu kumuua Chikane kwa kuitia sumu chupi yake.

Kesi hiyo imeelezwa kuwa mtihani mkubwa kwa kesi za kipindi cha kumalizika ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini zinazoendeshwa na maafisa ambao hawakusamehewa na tume ya ukweli na maridhiano.