1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jukwaa la Davos mwaka 2017

Sekione Kitojo
16 Januari 2017

Zaidi ya wanasiasa wa ngazi ya juu, viongozi mbali mbali wa kiuchumi na waansayansi wa masuala ya kiuchumi 3,000 wanatarajiwa mara hii kushiriki katika jukwaa la kiuchumi linalofanyika kila mwaka katika mjini Davos.

https://p.dw.com/p/2VsHr
Weltwirtschaftsforum in Davos
Nembo ya mkutano wa Davos mwaka huuPicha: World Economic Forum/Benedikt von Loebell

Katibu  mkuu  mpya  wa  Umoja  wa  mataifa  Antonio Guterres  naye ametangaza  atahudhuria  jukwaa  hilo.Mashirika  yote  muhimu  ya kimataifa  pia  nayo  yatawakilishwa  katika  mkutano  huo  wa  Davos. Lakini  mara  hii  kansela  wa  Ujerumani  ndie  atakayekosekana  katika jukwaa  hilo.

Klaus Schwab  hana  makosa. Na  hata  jukwaa  hilo  la  kiuchumi duniani  linalofanyika  mjini  Davos lililoasisiwa mwaka 1971 halina kosa. Lawama  pia  haziwezi  kuelekezwa  katika  ukosefu  wa  uwiano kiuchumi  katika  jamii  nyingi , pia  katika  ongezeko  la  hofu  kuhusiana na utandawazi, na  pia kukwama  kwa  maendeleo, matokeo ya kuwapo kwa  siasa  kali  za  mrengo  wa  kulia  katika  kura  ya  maoni  nchini Uingereza  iliyosababisha  nchi  hiyo  kujitoa  kutoka  Umoja  wa  Ulaya yaani  Brexit  na  uchaguzi  wa  rais  nchini  Marekani. 

Schweiz Klaus Schwab PK in Cologny bei Genf
Klaus Schwab muasisi wa jukwaa la kiuchumi la DavosPicha: Reuters/P. Albouy

Kwa  vyovyote  vile  iwavyo  mtu  angeweza  kufahamu  nukuu  hiyo , ambayo  Schwab  aliitoa   katika  mkutano  na  waandishi  habari wakati  wa  ufunguzi  wa  kikao  cha  47  cha  jukwaa  hilo  la  kiuchumi mjini  Davos.  Aliyategemea  baadhi  ya maandishi  yake ambayo aliyaandika  binafsi miaka  20  iliyopita.

Aliandika  wakati  huo  akionya  juu  ya  kuongezeka  kwa  siasa  kali  za mrengo  wa  kulia  na  kutoa  wito , kwamba  utandawazi  unapaswa kuwasaidia   watu  na  sio  tu  kwa  watu  wachache. Hali  hiyo inahitajika  hata  hii  leo.

Utandawazi

"Kila jaribio , Schwab  anasema , la  changamoto  zenye  utata  katika dunia hii zitakazotatuliwa  kwa  jibu  rahisi , litashindwa bila  shaka". "Hatupaswi  pekee  kuacha  suluhisho  lipatikane  kwa  njia  ya misimamo  mikali."  Jukwaa  lake  la  kiuchumi  duniani  analiona Schwab  kuwa  moja  kwa  moja  ni  mswada  mbadala.

Kila  mwaka  wanakusanyika  mjini  Davos  watu  wengi  wenye mawazo na mitizamo tofauti , wanasiasa , wafanyabaishara  na  wawekezaji , lakini  pia  wataalamu, asasi  za  kijamii  na  wanaharakati  wa  masuala ya  kijamii.  Na  kwa  hiyo  jukwaa  hilo  la  kiuchumi  linakuwa  ni mkusanyiko  wa  kila  mwaka  wa  viongozi  wa  juu  duniani  katika masuala  mbali  mbali.

Weltwirtschaftsforum in Davos
Watalii pamoja na washiriki wa kongamano la mjini Davos wakichanganyika kabla ya mkutano huoPicha: World Economic Forum/Benedikt von Loebell

Hapa  wanakutana  wanasiasa  wenye  madaraka  makubwa  duniani na  watu  wanaohusika  na  masuala  ya  kifedha.  Na  hapa  pia  kila mwaka  kunahubiriwa , kuhusu  utandawazi  zaidi, kufungua  mipaka  ya biashara  na  kuondoa  vizuwizi  vya  uwekezaji  wa  soko  la  hisa  ili kuiweka  dunia  katika  mahali  bora  zaidi.   Bila  shaka  hali  ya  zamani ya  uhakika  inaonekana   zaidi  na  zaidi  kuwa  inapotea.

Katika  mataifa  ya  magharibi  watu  tayari  wanajiuliza , iwapo utandawazi  pamoja  na  ushindano  wa  kimataifa  kama  umeleta mafanikio  yoyote.  Katika  kura  ya  kujitoa  Uingereza  katika  Umoja wa  Ulaya  hilo  lilichukua  katika nafasi  ya  juu, na katika  kuchaguliwa kwa  Donald Trump halikadhalika. Schwab  anatoa  wito  wa  kuwa  na mshikamano  na  uwiano.  "Kila  uchumi  wa  masoko anapatikana mshindi  na  mshindwa", anasema  Schwab.

Klausurtagung CDU-Bundesvorstand - Merkel
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Picha: picture-alliance-dpa/O. Dietze

Kansela hatahudhuria

"Kusimama imara  ndio  pekee  mfumo , ambao  mshindi  na  mshindwa watakuwa  na  mshikamano."  Kauli  mbiu  katika  mkutano  wa  mwaka huu  inasema, "Uongozi  wenye  uwajibikaji  na  unaoweza kubadilika kutokana  na  mahitaji". Ni dokezo  kuhusu  mtengano  unaoongezeka baina  ya  sehemu  kubwa  ya  wananchi  na  viongozi  wa  juu, na kukosekana  hali  ya  kuziamini  taasisi  mbali  mbali. 

Kansela  wa  Ujerumani Angela  Merkel  ametangaza  kutohudhuria jukwaa  hilo , kutokana  na  sababu  za  mipango  ya  matukio  mengine ya  kikazi. Badala  yake  waziri  wa  fedha  Wolfgang Schaeuble  na waziri  wa  ulinzi  Ursula von der Leyen  watakwenda  mjini  Davos. Rais wa  Ufaransa  Francois Hollande  atabakia  nyumbani, waziri  mkuu mpya  wa  Italia  Paolo Gentiloni  halikadhalika.

Belgien | EU-Gipfel | Theresa May
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa MayPicha: picture-alliance/Olivier Hoslet/EPA/dpa

Lakini waziri  mkuu  wa  Uingereza  Theresa May  atakuwapo , hataka kama  hakuna  mipango  kamili  kwa  ajili  ya  Brexit  ambayo inatarajiwa. Wanasiasa  muhimu  kutoka  Marekani  hawatakuwapo mwaka  huu, kwa  kuwa  Donald  Trump  ataapishwa  tarehe  20 Januari ambayo  ndio  siku  ya  mwisho  ya  kongamano  hilo.

Ni meneja  wa  zamani  tu  wa  mifuko  ya  uwekezaji  mbadala  Anthony Scaramucci  anatarajiwa , ambaye  ndie aliyetayarisha  sehemu  ya timu  ya  Trump  ya  kipindi  cha  mpito inayomtayarishia  hatua za kuingia  madarakani.

Mwandishi : Andreas Becker / ZR / Sekione  Kitojo

Mhariri: Iddi Ssessanga