1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya ya kimataifa yatakaa kutambua ushindi wa Gbagbo

Sekione Kitojo4 Desemba 2010

Jumuiya ya kimataifa inakataa kumtambua Laurent Gbagbo kuwa mshindi wa uchaguzi nchini Ivory Coast.

https://p.dw.com/p/QPVu
Rais Laurent Gbagbo akizungumza na waandishi habari.Picha: AP

Jumuiya  ya  kimataifa  inakataa  kumtambua   mshindi aliyetangazwa  katika   uchaguzi  mkuu  wa  rais  nchini  Ivory Coast Laurent  Gbagbo.  Umoja  wa  Ulaya, umoja  wa  mataifa  , pamoja na  Ufaransa  na  Marekani  zinamtambua  Alassane  Ouattara kuwa  ndie  mshindi  wa  uchaguzi  huo.  Jana  Ijumaa , baraza  la katiba  la  Ivory Coast  lilibadilisha   matokeo   ya  uchaguzi  huo ambayo  yameonyesha  kuwa  Ouattara  amepata   zaidi  ya  asilimia 54  ya  kura.  Wanaowaunga  mkono   wagombea  wote  wawili wameingia  mitaani   kuonyesha   uungaji  wao  mkono  na  hofu  ya kutokea  ghasia  bado  ipo  juu  baada  ya   watu  15  kuuwawa baada  ya  uchaguzi  huo. Jeshi  limefunga  mipaka  ya  nchi  hiyo ya  Afrika  magharibi  na  matangazo  ya  vyombo  vya  habari  vya kigeni  yamezuiwa.  Rais Laurent  Gbagbo  anatarajiwa  kuapishwa hii  leo  Jumamosi.

Elfenbeinküste / Wahl / Ouattara-Anhänger
Waungaji mkono wa kiongozi wa upinzani Alassane Ouattara wakishangilia ushindi.Picha: AP