1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Afisa wa polisi aachishwa kazi Afghanistan

29 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBe6

Serikali ya Afghanistan imemuachisha kazi mkuu wa polisi wa eneo ambako wahandisi wawili wa Kijerumani walitekwa nyara.Wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan imesema,afisa huyo amekiuka dhamana zake za kazi.

Kwa mujibu wa gazeti la Kijerumani “Bild am Sonntag,“ maiti ya mateka aliefariki wakati alikuwa amezuiliwa na wateka nyara,ina majeraha ya risasi katika magoti yote mawili na mgongoni. Hiyo huenda ikamaanisha kuwa mhandisi huyo aliekuwa na miaka 44,hakufariki kutokana na dhiki na hali ngumu ya kutekwa nyara.Hatima ya Mjerumani wa pili aliezuiliwa mateka tangu siku 11 zilizopita,bado haijulikani.