1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Mamia ya wanamgambo wa Taliban washambulia na kudhibiti mji wa kusini mwa Afghanistan.

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVi

Mamia ya wanamgambo wa Taliban wameshambulia na kuudhibiti mji wa Musa Qala, mji ambao wanajeshi wa Uingereza waliuondoka mwaka uliopita na kuwaachia viongozi wa kikabila kusini mwa Afghanistan.

Duru zinasema wanamgambo hao walinyakua silaha kutoka kwa polisi na pia wakaharibu makao makuu ya serikali katika mji huo.

Wakazi wanasemekana wamekuwa wakikimbia kutoka eneo hilo wakiogopa huenda majeshi ya NATO yakawashambulia kwa mabomu wanamgambo hao wa Taliban.

Maafisa wa NATO wamesema inaonekana kama kwamba wanamgambo hao walivamia makao hayo makuu ya serikali kulipiza kisasi cha shambulio la angani la juma lililopita lililosababisha kuuawa jamaa mmoja wa kiongozi wa kundi hilo la Taliban.