1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Rais Ahmadinejad azuru Afghanistan

14 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZC

Rais wa Iran, Mahmoud Ahmedinejad, anasema ana wasiwasi mkubwa juu ya madai ya Marekani na Uingereza kwamba Iran inawapelekea silaha wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kwanza nchini Afghanistan, rais Ahmedinejad amesema Iran inaunga mkono mchakato wa kisiasa unaoendelea nchini Afghanistan.

Ziara ya rais huyo inafanyika wiki moja baada ya rais wa Marekani, George W Bush, kusema wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari pamoja na rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, mjini Washington, kwamba Iran inahusika katika kuisambaratisha Afghanistan.

Rais Karzai hajayatilia maanani madai hayo akisema bado hayajathibitshwa.