1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Rais wa Afghanistan amelaani vifo vya raia

6 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLw

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan,amekosoa hatua zinazochukuliwa na vikosi vya kimataifa vya madola shirika kupambana na wanamgambo wa Kitaliban nchini humo.Amesema kuwa wanajeshi wanachukua hatua bila ya kuwa na uangalifu wa dhamana,kwani mara kwa mara raia wanauawa.Siku ya Jumatatu,tena raia 9 waliuawa karibu na mji mkuu Kabul,katika mashambulio ya angani yaliofanywa na vikosi vya kimataifa vinavyoongozwa na Marekani nchini Afghanistan.Watoto 3 ni miongoni mwa wananchi hao waliouawa.Tukio hilo linafuatia maandamano yaliofanywa na maelfu ya Waafghanistan siku ya Jumapili,mashariki mwa nchi baada ya hadi raia 8 kupigwa risasi.Mashahidi wamesema,vikosi vya Kimarekani vilifyatua risasi baada ya mshambulizi aliyejitolea muhanga kuvamia mlolongo wa magari yao.Maafisa wa Afghanistan na Marekani wamesema,matukio yote mawili yanachunguzwa.