1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Shambulio la kujitolea muhanga limeua watu 7

26 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpF

Si chini ya watu 7 wameuawa katika shambulio la kujitolea muhanga katika mji wa Urgun kwenye wilaya ya mashariki ya Paktika nchini Afghanistan.Shambulio hilo la bomu lililofanywa ndani ya mkahawa,vile vile limewajeruhi watu 19. Wakati huo huo,majeshi yanayoongozwa na shirika la kujihami la magharibi-NATO nchini Afghanistan yamesema,vikosi vyake siku ya Jumamosi,viliwaua kama wapiganaji 55 wa Taliban katika mapambano mawili mbali mbali yaliozuka kusini mwa nchi. Mwanajeshi mmoja wa NATO pia aliuawa,baada ya vikosi vinavyolinda amani katika wilaya ya kusini ya Uruzgan,kushambuliwa na kundi kubwa la wanamgambo.Mwaka huu,nchini Afghanistan,hadi hivi sasa machafuko yamechukua maisha ya kiasi ya watu 3,700-idadi hiyo ni mara nne zaidi kulinganishwa na mwaka jana.Wengi wao ni waasi,lakini inakisiwa kuwa kama raia 1,000 pia wameuawa katika machafuko hayo.