1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Wanajeshi wa Ujerumani washambuliwa tena.

9 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HD

Kumekuwa na shambulio jingine dhidi ya wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan. Msemaji wa wizara ya ulinzi mjini Berlin amesema kuwa kambi ya jeshi la Ujerumani Bundeswehr katika mji wa kaskazini mwa Afghanistan wa Kunduz imeshambuliwa kwa makombora mawili.

Hakuna mwanajeshi aliyejeruhiwa. Hii imekuja siku mbili baada ya wanajeshi watatu wa Ujerumani kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa muhanga katika mji wa Kunduz.

Wakati huo huo mhandisi raia wa Ujerumani anayeshikiliwa na wapiganaji wa Taliban tangu mwezi Julai ameiomba serikali ya nchi hiyo na Afghanistan kusaidia kupata kuachiliwa kwake. Katika video mpya iliyotolewa jana Jumatatu Rodolf Blechschmidt amesema kuwa aliachiliwa hivi karibuni na kukabidhiwa kwa shirika la kimataifa la msalaba mwekundu lakini alichukuliwa tena na wanamgambo wa Taliban.