1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Wanajeshi wawili wa NATO wauwawa

27 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoy

Nchini Afghanistan mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha amejiripuwa kwenye gari na kuuwa wanajeshi wawili wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO wakiwa kwenye msafara.

Mripuko huo umetokea mji wa kusini wa Kandahar kwenye barabara ambapo kuna majengo kadhaa ya serikali.Afghanistan iko katika kipindi cha hali mbaya kabisa ya umwagaji damu tokea vikosi vilivyoongozwa na Marekani kuupinduwa utawala wa Taliban hapo mwaka 2001 hali ambayo imekuwa ikikwamisha maendeleo na ujenzi mpya wa nchi hiyo.

NATO ilichukuwa majukumu ya usalama nchini Afghanistan kutoka Marekani mwaka huu na wanajeshi 32,000 walioko kwenye kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi kwa Usalama ISAF wako katika mapigano makali kabisa ya nchi kavu katika historia ya miaka 57 ya NATO.