1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul.NATO imejitoa kuwakingia kifua wanajeshi waliohusika na kisa cha fuvu la mwanaadamu.

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCz5

Jeshi la NATO hii leo limejitenga mbali na kundi la wanajeshi wa Ujerumani linalotuhumiwa kuhusika na kashfa ya fuvu la kichwa cha binaadamu nchini Afghanistan kwa kusema kuwa, kitendo chao kisichukuliwe kuwa ni hukumu kwa jeshi zima.

Jeshi la Ujerumani limefanikiwa kuwatambua wanajeshi sita wanaoshukiwa kucheza na fuvu hilo mnamo mwaka 2003, wakati walipokuwa katika jeshi la NATO.

Kiongozi wa jeshi la ISAF Jenerali David Richards amewaamuru wanajeshi wote wa jeshi hilo kujenga heshima kwa raia wa Afhganistan na imani zao.

Jeshi la ISAF limekubali kuiruhusu wizara ya ulinzi kufanyia uchunguzi kashfa hiyo ya fuvu la kichwa la binaadamu.