1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul.Uingereza yaondosha vikosi vyake huko mkoa wenye machafuko nchini Afghanista.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1y

Vikosi vya kijeshi vya Uingereza vimeondoshwa kutoka katika mkoa wenye machafuko kusini mwa Afghanistan, kufuatia ombi lililotolewa na wakuu wa kikabila katika eneo hilo.

Musa Qala aliyepo katika mkoa wa Helmand, amesema kuwa, mkoa huo ni sehemu mbaya zaidi katika nchi hiyo na kumeshuhudiwa mapigano makali kati ya vikosi vya NATO na wanamgambo wa Kitaliban.

Msemaji wa NATO amesema kuondoka kwao mkoani humo kunatokana na maombi ya Gavana wa mkoa huo.