1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamata kamata miongoni mwa wana wa ufalme Saudi Arabia

Oumilkheir Hamidou
6 Novemba 2017

Saudi Arabia inwaandama wana wa Ufalme, mawaziri na matajiri kwa dhana ya kuhusika na rushwa , katika mchujo usiokuwa na mfano, unaodhihirisha dhamiri ya mwanamfalme Mohammed Ben Salman ya kudhibiti hatamu za uongozi.

https://p.dw.com/p/2n5To
Saudi Arabien Kronprinz Mohammed bin Salman
Picha: Getty Images/AFP/F. Nureldine

Opereshini hiyo ya kutunisha misuli imesadifu wakati ambapo mwanamfalme Mohammed Ben Salmane, mwenye umri wa miaka 32, mtoto wa kiume wa mfalme Salmane, mwenye umri wa miaka 81, anazidi kujirundikia madaraka na kuleta mageuzi ya aina pekee katika sekta ya kiuchumi na pia kijamii katika nchi hiyo ya kihafidhina na ya kifalme.

Wimbi la kamata kamata linafuatia kuundwa tume mpya ya kupambana na rushwa inayoongozwa na mwenyewe mwanamfalme Mohammed ben Salman.

Miongoni mwa dazeni kadhaa ya wana wa ufalme na watu wengine mashuhuri waliokamatwa ni pamoja na tajiri mkubwa Al Walid Ben Tallal. Zaidi ya hayo mkuu wa kikosi chenye nguvu cha ulinzi wa taifa Metab ben Abdallah , mkuu wa jeshi la wanamaji Abdallah Al-Sultani na waziri wa uchumi Adel Fakih wameachishwa kazi kwa ghafla.

Mwanamfalme Al Walid bin Talal
Mwanamfalme Al Walid bin TalalPicha: picture-alliance/dpa/H. Ammar

 Kamata kamata inahusiana pia na kadhia zilizotokea zamani

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Al Arabiya, kinachogharamiwa na Saud Arabia, kwa jumla, wana  11 wa ufalme , mawaziri wanne na dazeni kadhaa za mawaziri wa zamani wamekamatwa huku tume ya kupambana na rushwa ikianzisha uchunguzi kuhusu kadhia ambazo baadhi zimetokea miaka chungu nzima iliyopita ikiwa ni pamoja na kadhia ya mafuriko yaliyoukumba mji wa Jeddah mwaka 2009 na kusababisha watu kadhaa kuuwawa-.

Mwanasheria mkuu wa Saud Arabia, Sheikh Saoud Al Mojeb ambae pia ni mwanachama wa tume ya kupambana na rushwa amesema "watuhumiwa watapatiwa haki sawa na kutendewa sawa na raia  yoyote yule mwengine wa Saud Arabia. Muda mfupi baadae wizara ya habari ikatangaza kufungwa akaunti za benki za wale wote waliotiwa mbaroni.

Hoteli ya Roseworld mjini Ryadh
Hoteli ya Roseworld mjini RyadhPicha: picture-alliance/dpa/A. Burgi

Watuhumiwa wanashikiliwa katoka hoteli ya anasa mjini Ryadh

Kupitia mitandao ya jamii ripoti zinasema watuhumiwa wote hao wanashikiliwa katika hoteli ya anasa ya Ritz Carlton ya mjini Ryadh."Kamata kamata hii inafungua enzi mpya ya siasa ya uwazi katika Ufalme wa Sauid Arabia" amesema waziri wa fedha Mohammed al-Jaddan.

Baraza la maulamaa-taasisi ya kidini yenye ushawishi mkubwa nchini humo, limesema mapambano dhidi ya rushwa ni muhimu sawa na mapambano dhidi ya ugaidi.

Kamatakamata ya mwishoni mwa wiki imetokea wiki mbili baada ya hotuba kali ya  mwanamfalme Mohammed Ben Salmane kwa jina la utani MBS katika kongamano la wawekezaji mjini Ryadh Oktober 24 iliyopita.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AP/Reuters

Mhariri . Mohammed Abdul-Rahman