1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Mtumbwi wazama Bugiri 30 wafariki

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuy

Zaidi ya watu 30 walifariki katika ajali ya mtumbwi kwenye eneo la Uganda la Ziwa Viktoria.Mtumbwi huo uliobeba abiria 69 ulizama mwishoni mwa juma na kulingana na polisi hakuna uwezekano wa kupata manusura zaidi.Boti hilo lilipinduka baada ya dhoruba kutokea.Kwa mujibu wa polisi idadi kubwa ya abiria vilevile matatizo ya kiufundi huenda yalichangia katika ajali hiyo kwenye eneo la kusini mashariki la Bugiri.

Abiria hao walikuwa safarini kuelekea sokoni wakati ajali hiyo ilipotokea.