1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni ya uchaguzi wa rais yaanza Rwanda

Josephat Nyiro Charo20 Julai 2010

Rais Paul Kagame amezindua kampeni ya chama chake katika mji mkuu, Kigali

https://p.dw.com/p/OQBe
Rais wa Rwanda, Paul KagamePicha: DW-TV

Shughuli za kampeni kwenye kinyang'anyiro cha Urais nchini Rwanda zimeanza leo rasmi nchini humo. Rais aliyeko madarakani na ambaye anagombea muhula mwingine kwenye uchaguzi huu, Paul Kagame, amewahakikishia raia wa nchi hiyo kuwa serikali itahakikisha kuwa uchaguzi huu utakaofanyika tarehe 9 mwezi ujao wa Agosti utaendeshwa kwa usalama, kwa haki na kwa uwazi.

Chama tawala cha RPF kimeanzia kampeni kwenye mji mkuu Kigali, huku wagombea wengine watatu wakipeleka kampeni zao mikoani. Uchaguzi huu unagombewa na watu wanne, baada ya vyama viwili vya upinzani kukataliwa usajiri. Wakati huo huo rais Kagame amefanya mkutano na waandishi wa habari mjini Kigali, na kuahidi kuwa endapo chama chake kitashindwa, ataachia madaraka bila kuchelewa.

Mwandishi: Daniel Gakuba

Mhariri: Abdul-Rahman