1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni za kura ya maoni kumalizika leo Kenya

Josephat Nyiro Charo2 Agosti 2010

Kambi ya Hapana kumaliza rasmi kampeni zake leo, baada ya upande wa Ndio kukamilisha kampeni zake hapo jana. Kivumbi kinatarajiwa hapo Agosti 4

https://p.dw.com/p/OZuU
Rais wa Kenya Mwai Kibaki, kulia, na waziri mkuu Raila OdingaPicha: AP

Kampeni za kuunga mkono na kupinga katiba mpya iliyopendekezwa nchini Kenya zinamalizika rasmi hii leo, ingawa hakutarajiwi kufanyika mikutano ya kusisimua. Jana upande unaoiunga mkono katiba mpya iliyopendekezwa ulikamilisha rasmi kampeni zake na leo upande unaopinga huenda ukawa na mkutano wake wa mwisho. Pande zote mbili, upande wa Ndio na Hapana, zina matumaini ya kushinda kura ya maoni kuhusu katiba hiyo itakayofanyika Jumatano wiki hii.

Mwandishi wetu Alfred Kiti kutoka mjini Naironi, ametuandalia taarifa hiyo.

Mwandishi:Alfred Kiti

Mhariri: Abdul-Rahman Mohamed