1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni za uchaguzi nchini Kenya

16 Januari 2013

Wakati wanasiasa nchini Kenya wakiendelea na kampeni zao kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Machi, suala la usalama bado linazusha mjadala na wasiwasi katika taifa hilo.

https://p.dw.com/p/17Km7
Raia wa Kenya wakati wakijiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi ujao
Raia wa Kenya wakati wakijiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi ujaoPicha: James Shimanyula

Kampeni zimeanzishwa kuwahamasisha wananchi kuzingatia umuhimu wa usalama wakati na baada ya uchaguzi, hii ni kufuatia kilichojitokeza baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo ghasia zilishuhudiwa takriban katika kila pembe ya taifa hilo la Afrika Mashariki. Hata hivyo waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu, miezi ya hivi karibuni kumekuwa kukishuhudiwa ghasia ambazo tayari wanasiasa wamekuwa wakinyooshewa kidole kwa kuzichochea jamii zao, yote hayo ni katika kuwania ushindi katika uchaguzi wa mwezi Machi. Je kuna uwiano gani kati ya kampeni na suala la usalama wakati au baada ya uchaguzi? Hilo ni miongoni mwa mengi ambayo Amina Abubakar amemuuliza Profesa Tom Namwamba mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Josephat Charo