1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini kuanza kutengeneza pete za ukeni za kuzuia VVU

30 Novemba 2023

Kampuni moja nchini Afrika Kusini imesema itaanza hivi karibuni kutengeneza mipira maalum ya kondom ya kuwalinda wanawake kupata maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi(VVU).

https://p.dw.com/p/4ZdRS
Close up of young man taking condom out of pocket in jeans. Remember about protection. Safe sex, AIDS. Pulling out condom gold color. Safety sex concept. Contraception. Contraceptive. World AIDS day
Afrika Kusini ni mmoja ya mataifa yalioathirika zaidi na VVU duniani.Picha: picture alliance/Zoonar

Kampuni ya afya ya Kiara iliyopo mjini Johannesburg itaanza kutengeneza vifaa hivyo katika miaka ijayo na inakadiria kutengeneza hadi kinga  milioni 1 kwa mwaka.

Hadi sasa kinga hiyo iliyotengenezwa mfano wa pete, karibu 500 zinapatikana kwa sasa kote barani Afrika na hutolewa bure kwa wanawake.

Aina hiyo ya kinga inayowekwa sehemu ya siri ya mwanamke, husambaza dawa inayozuia maambukizi ya VVU na tayari zimeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani WHO na katika nchi karibu kumi na mbili.

Kulingana na takwimu ya WHO, Virusi vya Ukimwi bado ni sababu kuu ya vifo kwa wanawake barani Afrika na asilimia 60 ya maambukizi mapya hutookea kwa wanawake.