1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kandanda. Bundesliga yazidi kupamba moto.

2 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTd

Katika michezo ya ligi daraja la kwanza nchini Ujerumani, Bundesliga , jana Jumamosi, Werder Bremen iliichapa Eintracht Frankfurt kwa mabao 2-1, Hertha BSC Berlin iliibwaga chini Wolfsburg kwa mabao 2-1 nayo, wakati Hanover iliisimamisha Bochum kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2.

Cottbus na Nuremberg ziligawana points baada ya kutoka sare ya bao 1-1, wakati Borussia Dortmund ilipata ushindi wake wa pili mfululizo msimu huu kwa kuishinda Hansa Rostock kwa bao 1-0. Duisburg iliigaragaza Arminia Bielefeld kwa mabao 3-0.

Leo Bayern Munich inakumbana na HSV Hamburg , wakati mabingwa Stutgart inakwaana na Karlsruhe SC iliyopanda daraja msimu huu.