1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela aonya kuhusu hali ya wasi wasi wa kiuchumi.

1 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CieJ

Berlin.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameonya kuwa kuna hali inayoendelea ya wasi wasi wa kiuchumi kutokana na mambo mbali mbali yanayotokea duniani, na kuahidi kuwa uchumi wa nchi yake ukiwa ndio mkubwa katika bara la Ulaya utaendelea na juhudi zake za mageuzi ili kupambana na ukosefu wa ajira. Katika hotuba yake ya mwaka mpya, Merkel amesema kuwa mwaka 2007 ulikuwa wa mafanikio kwa Ujerumani, akisisitiza kuwa kwa mara ya kwanza tangu kuungana kwa Ujerumani mbili, mwaka 1990, nchi hiyo imefikia karibu ya kuweka wizani sawa katika bajeti na kuimarisha nafasi yake katika utafiti na elimu. Merkel ameonya kuwa idadi ya watu milioni 3.5 ya watu wasiokuwa na kazi nchini Ujerumani bado ni ya juu sana na mapambano dhidi ya ukosefu wa ajira yanabaki kuwa moja kati ya malengo makuu katika mwaka 2008. Katika kiwango cha kimataifa , kansela wa Ujerumani amesema kuwa nchi hiyo imechukua jukumu la changamoto ya kusaidia kuweza kuufanya umoja wa Ulaya kuwa na uwezo wa kuchukua hatua , kufuatia makubaliano katika mkataba wa kihistoria wa kufanyia mageuzi katiba ya umoja huo.