1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merkel amalizia ziara yake nchini Mexico

Castrititus, Michael / Mexico Stadt (RBB) NEU20 Mei 2008

Kansela Merkel asema aridhika na ziara yake ya wiki moja Latin Amerika

https://p.dw.com/p/E32d
Kansela Merkel na rais wa Mexico CalderonPicha: AP


Kansela Angela Merkel amemaliza ziara yake ya kwanza ya wiki moja katika nchi za Latin Amerika  jana kwa kuitembelea Mexico.Alikutana na rais Felipe Calderón na kuzungumzia juu ya kishindo kinachosababishwa na kuzidi kupanda bei za vyakula ulimwenguni.


Licha ya urafiki ulioko kati yao,katika suala la kupanda bila ya kiasi bei za vyakula ulimwenguni,msimamo wa kansela Angela Merkel unaonyesha kutofautiana sana na ule wa rais Calderón wa Mexico.


Rais Calderón amezitaka Marekani na Umoja wa ulaya zifutilie mbali ruzuku wanazolipwa wakulima ili wakulima maskini wa nchi yake waweze kushindana kibiashara.


Kwa mfano maahindi yanayoruzukiwa sana na Marekani yamesheheni katika masoko ya Mexico na kwa namna hiyo kusababisha kufilisika wakulima wadogo wadogo wa nchi hiyo na baadhi yao kulazimika kuyapa kisogo masakani yao na kuhamia katika nchi jirani ya kaskazini.Bei ya mahindi ilipopanda mwaka jana kutokana na kuongezeka mahitaji ya nafaka hiyo ili kutengeneza mafuta,Wamexico walikumbwa na shida japo kwa muda ya kujipatia chakula chao maarufuTortilla.Kansela Angela Merkel amefifiisha lakini matumaini ya kufikiwa makubaliano haraka ya kufutiliwa mbali marupu rupu wanayolipwa wakulima akigusia juu ya kukwama mazungumzo ya shirika la biashara ulimwenguni WTO.


"Tumeahidiana kwamba umoja wa Ulaya upunguze ruzuku hadi ifikapo mwaka 2013.Na ndio maana tumesema tunataka mada hii iiorodheshwe katika ajenda ya mazungumzo.Nnahisi ni muhimu pia kuzungumzia suala hilo wakati wa mkutano kati ya mataifa manane tajiri ya kiviwanda na matano yanayonyanyukia.Hatuwezi sisi peke yetu kupanga bei za vyakula.Lakini tunaweza kubuni mikakati ya kutathimini mahitaji ya chakula ili kuweza kuelekeza ipasavyo sera zetu za maendeleo na kuwajibika zaidi."


Mexico ni kituo cha mwisho cha ziara ya wiki nzima ya kansela Angela Merkel katika nchi nne za Latin Amerika.Mbali na  mada hiyo ya kupanda kwa bei za vyakula ulimwenguni,kansela Angela Merkel na wenyeji wake ,nchini Brazil,Peru,Columbia na hatimae jana nchini Mexico,walizungumzia pia kuhusu juhudi za kupambana na madawa ya kulevya na matumizi ya nguvu.


Kansela Angela Merkel ambae hivi sasa yuko njiani kurejea nyumbani mjini Berlin amesema ameridhishwa na matokeo ya ziara yake akihimiza tunanukuu:"ni jambo la maana tukiimarisha zaidi uhusiano jumla pamoja na Latin Amerika.Mwisho wa kumnukuu