1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karadzic mahkamani tena.

29 Agosti 2008

Karadzic haikuitikia hatia akifikishwa tena leo Mahkamani.

https://p.dw.com/p/F7HI
KaradzicPicha: AP

Mahkama ya Umoja wa Mataifa, inayohusika na uhalifu wa vita katika ile iliokua Yugoslavia ilitoa jibu la kutokua na hatia kwa niaba ya mshtakiwa kiongozi wa zamani wa Bosnia wa ki-serbia, Radovan Karadzic.

Karadzic anashtakiwa mashtaka ya uhalifu wa kivita na ya kuhilikisha umma wakati wa vita vya Bosnia kati ya 1992-95.

►◄

Katika kikao chake cha pili cha kusikiliza iwapo anakubali hatia au la juu ya mashtaka hayo na uhalifu dhidi ya binadamu,Karadzic alikeataa kujibu mashtaka hayo yote yanayomkabili.

Matokeo yake, hakimu wa mashtaka Iain Bonomy aliamua kwa niaba yake kujibu "hakubali makosa" juu ya mashtaka yote.

Karadzic alifika mahkamani mjini The Hague, akivaa suti nyeusi na alianza kwa kuelezea nia yake ya kujitetea mwenyewe.

Katika kikao cha kwanza cha mashtaka mwezi uliopita, pia karadzic alikataa kujibu ni mkosa au la.Badala yake alitoa changamoto juu ya uhalali wa Mahkama inayomshtaki.

Mashtaka dhidi ya Karadzic mwenye umri wa miaka 63,yanajumuisha mawili -moja kuhilikisha umma wa wsaislamu 8000 wa Bosnia huko Srebrenica na kuuzingira mji mkuu Sarajevo kwa muda wa miezi 43.

Mashtaka haya yanatarajiwa kuanza mwakani baada ya taratibu zote za kesi yake kukamilishwa.

katika tamko lake la karibuni, Karadzic ameukosoa mfumo unaomshtaki yeye akidai umeelemea upande mmoja na si wa haki ukitaka tu kumkuta na hatia.Alikariri hoja yake kuwa Marekani imetia nia ya kumhilikisha.

Akiwa ametiwa mbaroni hapo julai mwaka huu mjini Belgrade,alidai mpatanishi wa wa amani wa vita vya Bosnia,muamerika Richard Holbrooke pamoja na aliekua waziri wa nje wa Marekani Madeleine Albright,wafikishwe pia mahkamani kuhojiwa.

Karadzic anadai kuwa Holbrooke amevunja ahadi aliyompa kwamba hataguswa na sasa anataka kumuona ananyongwa.Haya ni mashtaka ambayo,mjumbe huyo wa zamani wa kibalozi wa Marekani akikanusha mara kwa mara kutoa ahadi hiyo.

Mabingwa wa sheria wanalinganisha sasa kesi ya Karadzic kwenda sambamba na ile ya marehemu rais wa zamani wa yugoslavia,Slobodan Milosevic baada ya kufikishwa mahkamani mjini The Hague hapo 2001 kukabili pia mashtaka ya kuhilikisha umma.