1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Mafunzo

Karandinga: Familia Inayojali

Grace Kabogo
2 Februari 2022

Mimba nyingi sana kwa wakati mfupi zimesababisha Linda Malongo kuishiwa nguvu. Madai ya mama mwenye miaka 20 hayakuchukuliwa kwa uzito na mumewe, Tommy, ambaye alisisitiza kupata mtoto wa kiume na mwishowe Linda akafa.

https://p.dw.com/p/46PEX
Crime Figters Episode 6 Family Planing
Picha: DW

Hadi hivi karibuni, Tommy hakuelewa kwa nini wanawake wanahitaji muda wa kupumzika kati ya uzazi na uzazi na kwamba mimba ambazo hazikupangwa zinaweza kusababisha afya ya mama na mtoto kuwa hatarini. Akiwa ameketi chini ya mpapai nyuma ya nyumba yake, Tommy anatusimulia hadithi yake, akitamani kurudisha nyuma muda. Mchezo huu wa Karandinga unajadili faida za uzazi wa mpango, haki ya wanawake kuamua kuhusu miili yao wenyewe na umuhimu wa wanaume na wanawake kuishi pamoja kwa usawa. Hadithi hii imeandikwa na Marta Barroso kutoka Msumbiji

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi

Onesha taarifa zaidi