1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katiba mpya nchini Kenya yajadiliwa

17 Novemba 2009

Huenda wananchi wa Kenya wakawa na katiba mpya ya nchi yao hapo mwakani, jambo ambalo wamelililia kwa muda mrefu.

https://p.dw.com/p/KZBC
A Maasai woman cast her ballot, Monday, Nov. 21, 2005 near Kajiado, some 100 kilometers south of the capital Nairobi during the referendum on a draft constitution .Thousands of Kenyans lined up to vote Monday in a referendum on a draft constitution that spells out how East Africa's largest economy will be run and its resources shared.(AP Photo/Karel Prinsloo)
Wananchi wa Kenya wakipiga kura kuhusu katiba ya nchi yao hapo mwaka 2005Picha: AP

Jana mswada wa katiba hiyo ulichapishwa, na wananchi sasa wamepewa mwezi mmoja kuujadili na kutoa maoni yao kwa kamati ya mabingwa ambao walioitunga hati hiyo.Mwenyekiti wa kamati iliotunga mswada huo, Nzamba Kitonga, alisema huo ni mswada wa kuweza kuweko mdahalo miongoni mwa Wakenya. Miongoni mwa mapendekezo ya mswada huo ni kuwa na waziri mkuu mwenye madaraka ya utendaji, mabaraza mawili ya bunge, madaraka yasambazwe mikoani na vijijini, kubakishwe mahakama za Kiislamu za kadhi, na kwamba mawaziri wa serikali wasizidi 20, nusu yao wakitokea nje ya bunge.

Baada kuchapishwa mswaada huo, Othman Miraji alifanya mahojiano ya simu na waziri wa Kenya wa sheria na masuala ya katiba, Mutula Kilonzo: vipi anavoutathmini mswada huo.

Mtayarishaji: Othman Miraji

Mpitiaji: Mohamed Abdulrahman