1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya Airways kuruka moja kwa moja hadi Marekani

Bruce Amani
24 Februari 2017

Ndege za Kenya zimepewa kibali cha usalama na maafisa wa Marekani kuanza safari za ndege za moja kwa moja hadi Marekani.

https://p.dw.com/p/2YCJv
Kenya Airways Flughafen Nairobi ARCHIV
Picha: picture-alliance/dpa

Waziri wa Uchukuzi wa Kenya, James Macharia, alisema kibali hicho kimetokana na kuimarishwa kwa miundombinu katika uwanja mkuu wa ndege mjini Nairobi.

Macharia alisema Kenya inatumai kuwa hatua hiyo itaimarisha biashara kati yake na Marekani na kuongeza mgawo wake wa watalii wa Marekani wanaotembelea nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Serikali ina hisa katika shirika la ndege la Kenya Airways na hivi karibuni ilimaliza kujenga kituo kipya cha abiria katika uwanja huo na inapanga kutumia fedha zaidi katika kuuboresha Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.