1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni ya ‘Usinitoe Utamu'

Wakio Mbogo17 Desemba 2018

Kenya: Kupitia kampeni iliyopewa jina ‘Usinitoe Utamu’, wadau wanawatumia vijana, waathiriwa pamoja ngariba walioiasi kazi hiyo ya ukeketaji, kuhimiza kukomeshwa kwa mila hiyo.

https://p.dw.com/p/3AFmf

Ipo haja ya kuhimiza juhudi za ujumla ili kufanikisha vita dhidi ya ukeketaji hasa katika maeneo ya vijijini. Ni wito unaotolewa na mashirika ya kijamii nchini Kenya, yalio na mtazamo kuwa iwapo serikali itayaleta pamoja makundi ya watu wanaoathiriwa na ukeketaji kwa njia moja au nyingine, basi ukeketaji utaweza kutokomezwa. Kupitia kampeni iliyopewa jina ‘Usinitoe Utamu’, wadau hawa wanawatumia vijana, waathiriwa pamoja ngariba walioiasi kazi hiyo ya ukeketaji, kuhimiza kukomeshwa kwa mila hiyo.