1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya kuuza mafuta nje

Mohammed Khelef
2 Agosti 2019

Kenya inajiandaa kuuza nje mafuta ghafi baada ya kupata mnunuzi wa mapipa 200,000 yaliyo na thamani ya dola milioni 12 za Marekani.

https://p.dw.com/p/3NEES
Öltanker | Alaskan Frontier BP
Picha: picture-alliance/AP Photo/A. Grillo

Hii itakuwa shehena ya kwanza ya mafuta ghafi yatakayouzwa nje ifikapo kipindi cha robo ya mwisho ya mwaka 2019.

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni ya Tullow, mafuta hayo tayari yameshasafirishwa hadi mjini Mombasa.

Tullow Oil, iliyo na visima vya mafuta katika Kaunti ya Turkana, imekuwa ikisafirisha mapipa 600 ya mafuta kwa siku hadi eneo la pwani ya Kenya ila tangu mwezi wa Mei imeiongeza idadi hiyo na kufikia mapipa 2,000.

Hata hivyo maelezo ya kampuni iliyoingia ubia na Kenya hayajakuwa bayana.

Kenya iligundua hifadhi ya mafuta mnamo 2012 kwenye Bonde la Lokichar na inakisiwa kiasi ya mapipa milioni 560 huenda yakapatikana baada ya eneo hilo kuchimbwa kikamilifu.
 

Thelma Mwazdaya/DW Nairobi