1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Uchunguzi wa kifo cha Mutula Kilonzo wafanyika leo

29 Aprili 2013

Serikali ya Kenya hii leo 29.04.2013 imeanza uchunguzi rasmi kujua nini kilisababisha kifo cha seneta wa eneo la Makueni nchini humo Mutula Kilonzo.

https://p.dw.com/p/18Ora
Marehemu Mutula Kilonzo(katikati)
Marehemu Mutula Kilonzo(katikati)Picha: AP

Kulingana na Mtaalamu wa uchunguzi wa sababu za kifo Johansen Oduor amesema uchunguzi huo kwa sasa utajikita zaidi katika chakula cha mwisho alichokula Marehemu Kilonzo..

Mutula Kilonzo ambaye alikuwa waziri katika serikali iliopita, alikutwa chumbaniJumamosi asubuhi akiwa amefariki huku mapofu yakimtoka mdomoni na puani. Msemaji wa familia yake Chris Musau amesema mipango ya mazishi itafanyika wakati ukapomalizika.

Jee wa kenya watamkumbuka vipi marehemu Mutula Kilonzo? Amina Abubakar amezungumza na Professa Tom Namwamba ambaye ni mchambuzi wa maswala ya kisiasa akiwa Nairobi na kwanza ana haya ya kueleza. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman