1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya mauaji dhidi ya Pistorius yaahirishwa

Abdu Said Mtullya19 Februari 2013

Kesi ya kusikiliza ombi la kuachiwa kwa dhamana bingwa wa michezo ya Olimpiki ya walemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, imeahirishwa hadi Jumatano ili kutoa muda kwa waendesha mashitaka kupitia hati ya maelezo.

https://p.dw.com/p/17gvk
"Blade Runner" Oscar Pistorius awaits the start of court proceedings in the Pretoria Magistrates court February 19, 2013. Pistorius, a double amputee who became one of the biggest names in world athletics, was applying for bail after being charged in court with shooting dead his girlfriend, 30-year-old model Reeva Steenkamp, in his Pretoria house. REUTERS/Siphiwe Sibeko (SOUTH AFRICA - Tags: CRIME LAW SPORT ATHLETICS TPX IMAGES OF THE DAY)
Mwanariadha Oscar Pistorius kizimbaniPicha: Reuters

Hatua hiyo inatokana na waendesha mashitaka kutaka muda zaidi kusoma maelezo yaliyowasilishwa na upande wa utetezi. Awali kesi hiyo ilipokuwa ikisikilizwa leo mshitakiwa alisema hakudhamiria kumuua mpenzi wake mwanamitindo, Reeva Steenkamp. Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo ya Oscar Pistorius, ambaye ameshtakiwa kwa tuhuma za kumuuwa mpenzi wake kwa kudhamiria. Mwendesha mashtaka aliiambia mahakama ya mjini Pretoria kuwa Pistorius alimpiga risasi mpenzi wake mara nne.

Mwendesha mashtaka, Gerrie Nel, aliiambia mahakama kuwa Pistorius alifyatua risasi kupitia kwenye mlango wa kuingilia bafuni katika nyumba yenye ulinzi mkali na kumuua mpenzi wake mwanamitindo, Reeva Steenkamp, aliyekuwa na umri wa miaka 26. Mwendesha mashtaka huyo pia aliiambia mahakama kwamba mlango wa kuingilia bafuni ulikuwa umevunjwa.

Mwendesha mashtaka alisema, wakati Pistorius akiwa anatoa machozi ya kimya kimya, kwamba mshtakiwa, Pistorius, aliinuka kutoka kitandani na kuipachika miguu yake ya bandia, na alianza kutembea kiasi cha umbali wa mita saba kutoka chumbani, kuelekea bafuni na kufyatua risasi.

South African "Blade Runner" Oscar Pistorius (R) talks to his father Henke after his court appearance in Pretoria February 15, 2013. Pistorius, a double amputee who became one of the biggest names in world athletics, broke down in tears on Friday after he was charged in court with shooting dead his girlfriend, 30-year-old model Reeva Steenkamp, in his Pretoria house. REUTERS/Stringer (SOUTH AFRICA - Tags: SPORT ATHLETICS CRIME LAW) NO SALES. NO ARCHIVES. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. IT IS DISTRIBUTED, EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS. SOUTH AFRICA OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN SOUTH AFRICA
Mwanariadha Oscar Pistorius kizimbaniPicha: Reuters

Dhamira ya mauwaji

Mwendesha mashtaka huyo aliiambia mahakama kwamba Pistorius aliua kwa kudhamiria kwa sababu tokea mwanzo alipanga kusema kwamba alifikiri alikuwa anamuua mwivi. Mwendesha mashtaka, Gerrie Nel, aliiambia mahakama kuwa Pistorius alipanga kila kitu mapema, na aliuliza kwani nini mwivi ajifungie bafuni?

Lakini wakili wa Pistorius, Barry Roux, ameyakana mashtaka ya kuua kwa kudhamiria. Wakili huyo aliiambia mahakama kwamba ufyatuaji wa risasi ulikuwa ni tukio la ajali na wala siyo mauaji. Wakili huyo amesema hakuna ushahidi wa mauaji.

Mshatakiwa Pistorius alifikishwa mahakamani mjini Pretoria leo kusikiliza uamuzi wa mahakama iwapo anaweza kuachiwa kwa dhamana. Akitetea hoja ya mteja wake kuachiwa kwa dhamana, wakili Barry Roux alisema kuwa Pistorius, mwenye umri wa miaka 26, hana mashtaka mengine yanayomkabili. Mwanamichezo Pistorius, anayetumia miguu bandia katika kukimbia, mwaka jana alikuwa mtu wa kwanza aliyekatwa miguu yote miwili kushiriki katika mashindano ya michezo ya olimpiki.

Shughuli za maziko zafanyika

Wakati kesi ya Pistorius ikiendelea katika mji wa Pretoria, aliyekuwa mpenzi wake, Reeva Steenkamp, alikuwa anafanyiwa maziko katika mji wa Port Elizabeth. Mwili wake ulipelekwa kwenye kanisa dogo. Jeneza lake lililopambwa kwa maua lilibebwa na watu sita na kupelekwa kwenye sehemu ya kuchomwa moto. Watu waliokuwa wamejawa majonzi waliwasili kwenye maziko yaliyokuwa ya faragha katika mji wa Port Elizabeth.

In this Nov. 4, 2012 photo, South African Olympic athlete Oscar Pistorius and Reeva Steenkamp, believed to be his girlfriend, at an awards ceremony, in Johannesburg, South Africa. Olympic athlete Oscar Pistorius was taken into custody and was expected to appear in court Thursday, Feb. 14, 2013, after a 30-year-old woman who was believed to be his girlfriend was shot dead at his home in South Africa's capital, Pretoria. (AP Photo/Lucky Nxumalo-Citypress) SOUTH AFRICA OUT
Pistorius (kulia) na mpenzi wake ReevaPicha: picture-alliance/AP

Marehemu, aliyekuwa msanii wa kuonyesha mitindo na aliyekuwa anasomea sheria, alikuwa na umri wa miaka 29. Aliuawa siku ya wapendanao, Valentine's Day - Februari 14. Mama yake, June Steenkamp, amesema anataka kujua kwa nini ameuliwa? Mama huyo aliuliza kwa nini Pistorius alifanya hivyo? Wakati huo huo wataalamu wa sheria wamesema kuwa kesi ya Pistorius ambayo imeahirishwa itachukua muda mrefu.

Mwandishi:Mtullya Abdu/afpe,rtre
Mhariri: Josephat Charo