1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kesi ya rushwa dhidi ya kampuni ya Shell na Eni yaanza

Sekione Kitojo
14 Mei 2018

Katika mji wa Milan nchini Italia inaanza kesi ya rushwa dhidi ya wafanyakazi wa kampuni za mafuta za Shell na Eni. Pia mjini Lagos  kesi nyingine itafanyika iliyofikishwa mahakamani na kundi la walinzi wa mazingira.

https://p.dw.com/p/2xft6
Ölpreisrutsch führt auch bei Shell zu Gewinneinbruch
Picha: picture-alliance/dpa/PA Wire/Yui Mok

Mashitaka  hayo  yanalengo  la  kutaka  leseni  za  makampuni  hayo zifutwe.

Mji  wa  Milan  nchini  Italia  kuanzia  leo  utakuwa  sehemu  ya jukwaa  la  mwezi  mzima  litakalojishughulisha  na  kuweka  wazi biashara  chafu   katika  sekta  ya  mafuta. Mwendesha  mashtaka wa  mji  wa  Milan  nchini  Italia  anataka  kuyawajibisha  makumpuni ya  Eni  la  Italia  pamoja  na  Shell  la  Uingereza, kwa  kutoa  hongo ya  mamilioni  ya  fedha  ili  kupata  leseni  ya  kufanyakazi  nchini Nigeria.

Nigeria Explosion Pipeline in Ogun
Eneo linalochimbwa mafuta la Ogun nchini Nigeria Picha: picture-alliance/AP Photo/S. Alamba

Watu 15  wanashitakiwa, wengi  wao  wakiwa  wafanyakazi  wa makampuni  hayo  mawili , kwa  kuhusika  na  rushwa.

Sio  tu  katika   mji  wa  Milan ambako  makampuni  hayo yatakabiliwa  na  kesi, lakini  pia  mjini  Lagos  kutakuwa  na  kesi nyingine  dhidi  ya  makamuni  hayo  makubwa  ya  mafuta.

Katika  kesi  hiyo  mjini  Lagos  makampuni  hayo yatakabiliwa  na kesi  iliyofikishwa  mahakamani  na  makundi  ya  haki  za  binadamu HEDA, Human and Environmental Development Agenda,  ajenda kwa  ajili  ya  maendeleo  ya  watu  na  mazingira  dhidi  ya makampuni  hayo. HEDA  inataka  kampuni  ya  Shell  na  Eni  ifutiwe leseni  zao. Kesi  hizo  zote  zinahusu  matukio  yaliyotokea  mwaka 2011.

Nigeria Niger Delta Ölverschmutzung Öl
Kituo cha kusukuma mafuta cha Shell katika jimbo la Niger Delta nchini NigeriaPicha: Getty Images/C. Hondros

Rushwa na  ubadhirifu

Wakati  huo  kampuni  za  Shell  na  Eni zililipa  kiasi   cha  dola  za Marekani bilioni  1.3 katika  akaunti  ya  serikali  ya  Nigeria. Kwa kiwango  hiki  cha  fedha  makampuni  hayo  yalitaka  kupata uhakika wa  kumiliki  kitalu  cha  mafuta  namba  OPL 245 ,  kitalu ambacho  kwa  maelezo  ya  makampuni  hayo  kinaweza  kutoa mafuta  yenye  thamani  ya  hadi  dola  bilioni  3. Kiasi  kikubwa  cha fedha  hizo kilitumbukia  sio  katika  hazina  ya  serikali  ya  Nigeria , badala  yake   zilikwenda  katika  kampuni  ya  Maluba inayojishughulisha  na  mafuta  na  gesi.

Nigeria Port Harcourt Arbeiter auf Plattform Ölförderung
Mfanyakazi wa kampuni ya mafuta akikagua mitambo nchini NigeriaPicha: Getty Images/AFP/P. Utomi Ekpei

Serikali  ya  Nigeria  tayari  imekwisha  jieleza  katika  kesi iliyofanyika  nchini  Uingereza , kwamba  ununuzi  wa  leseni  hiyo kwa  ajili  ya  eneo  hilo  kubwa  la  mafuta  mwaka  2011 ni  kinyume na  sheria, amesema  msemaji  wa  kundi  la  HEDA Lanre Suraju katika  mahojiano  na   DW. Kutokana  na  fedha  hizo  za  ununuzi dola  milioni 520  zilikuwa  taslimu  na  kwamba  ni  fedjha  za  rushwa zilizogawanywa  kwa  wanasiasa.

 

Serikali  hata  hivyo  iliambulia  kiasi  cha  dola  milioni  210  tu. Mhusika  mkuu  katika  kampuni  ya  Malabu Oil & Gas  ni  Dan Etete , ambaye  katika  miaka ya  1990  alifanyakazi  chini  ya utawala  wa  dikteta  Sani  Abacha kama  waziri  wa  mafuta.

Nigeria Dan Etete
Waziri wa zamani wa mafuta wa Nigeria Dan Etete (kulia)Picha: picture-alliance/dpa/G. Barbara

Katika  wadhifa  huo  aliwahi  mwaka  1998  kupata  leseni ya kuchimba  mafuta  na  kuihamishia  katika  kampuni  yake. Etete alihukumiwa  mwaka  2007  nchini  Ufaransa  kwa  kufanya  biashara haramu  ya  fedha . Alipaswa  pia   kufikishwa  mahakamani  mjini Milan, lakini  kwa  mujibu  wa  Lanre Surahu , Etete  kwa  sasa hajulikani  aliko.

Mwandishi: Martina Schwikowski /ZR/  Sekione  Kitojo

Mhariri: Iddi Ssessanga