1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Khaftar akataa kusaini makubaliano ya kusitisha vita

14 Januari 2020

Shirika la habari la Urusi la TASS limeripoti kuwa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo imesema kuwa mbabe wa kivita Khalifa Haftar ameondoka Urusi bila kutia saini makubaliano ya kusitisha vita.

https://p.dw.com/p/3W9xZ
Libyen Khalifa Haftar
Picha: AFP/A. Doma

Hapo awali Waziri wa nchi za kigeni wa urusi Sergey Lavrov alikuwa amesema kuwa sehemu kubwa ya wahusika katika machafuko ya Libya wametia saini makubaliano ya kusitisha mapigano isipokuwa jenerali Haftar na rafiki yake Aguila Saleh ambaye ni spika wa bunge la mashariki mwa Libya lililojitenga.

Lavrov alisema Haftar na Aguila walitaka wapewe muda zaidi hadi asubuhi ya Jumanne ndiposa waweze kutia saini makubaliano hayo ingawa kwa sasa mbabe huyo anadaiwa kuondoka Urusi tayari.

Haftar ambaye anaongoza jeshi linalojiita jeshi la kitaifa la Libya ni sehemu muhimu ya machafuko hayo.

Pande hizo zinazozana zinatarajiwa mjini Berlin baadae mwezi huu ingawa msemaji wa serikali ya Ujerumani Stffen Seibert amesema tarehe ya mkutano huo haijawekwa.

Vikosi vya Haftar vimekuwa vikipigania kudhibiti mji mkuu Tripoli ambao uko chini ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.