1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiasi cha watu watano wauwa katika ghasia dhidi ya wageni

18 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E23Q

JOHANNESBERG

Kiasi cha watu watano wamechomwa moto au kupigwa hadi kufa katika mji wa Jonannesberg nchini Afrika Kusini katika ghasia zinazoendelea dhidi ya wahamiaji.

Zaidi ya watu wengine 50 wamepelekwa hospitali katika mji wa Cleveland kufuatia majeraha ya risasi au kudungwa visu.Ghasia dhidi ya wageni nchini humo zilianza wiki moja iliyopita katika mji wa Alexandra ambapo wahamiaji kutoka nchi mbali jirani za Afrika walikuwa wakivamiwa na kupigwa aidha kwa risasi au mapanga na makundi ya vijana wa Kiafrika kusini ambao wanadai lazima wageni wafukuzwe kutoka nchini humo.Raia wakigeni kutoka nchi za Zimbabwe,Msumbiji na Malawi wamekimbilia usalama katika vituo vya polisi.Shirika la msalaba mwekundi nchini humo sasa linatoa msaada wa chakula na mablanketi ya kulalia kwa mamia ya wahamiaji waliojawa na uoga ambao wamelazimika kuhama nyumba zao.