1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI: Rais wa zamani aachiliwa kutoka gerezani

6 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCC5

Rais wa zamani wa Rwanda Pasteur Bizimungu ameachiliwa huru kutoka gerezani alikokuwa anatumikia kifungo cha miaka 15 kwa makosa yaliyochangia uhasama wa kikabila na matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Kuachiliwa kwa kiongozi huyo wa zamani kumetokea siku moja tu kabla ya kuadhimisha miaka 13 tangu mauaji ya kikabila ya Rwanda yalipofanyika.

Pasteur Bizimungu alihukumiwa mwezi juni mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia, mahakama nchini Rwanda mwaka jana ilitupilia mbali rufani aliyoiwasilisha pamoja na waziri wa zamani wa usafiri Charles Ntakiruthika ambae alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.

Wakili wa bwana Bizimungu amesema kuwa amefurahishwa na uamuzi wa kumsamehe mteja wake.