1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI.Ufaransa inatuhumiwa kuwasaidia wanajeshi waliotekeleza mauaji ya halakini ya mwaka 1994

25 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzZ

Rwanda imeanzisha uchunguzi dhidi ya vikosi vya Ufaransa vinavyo kabiliwa na tuhuma za kuwasaidia wanajeshi waliotekeleza mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Rais wa Rwanda Paul Kagame wa kabila la Tutsi ambae alitwaa madaraka baada ya mauaji hayo ya halaiki ameilaumu Ufaransa kwa kuwapa mafunzo na silaha wapiganaji wa ki Hutu ambao walihusika zaidi na mauaji yaliyoendelea kwa siku mia moja nchini Rwanda.

Wanyarwanda laki nane wengi wao wa kabila la Tutsi na wa-Hutu wachache waliokuwa na msimamo wa kadiri waliuwawa.

Tume ya wawakilishi saba itaanza kusikiliza ushahidi wa watu ishirini kuanzia wiki ijayo kutathmini hatua za kisheria zinazotarajiwa kuchukuliwa na serikali ya Kigali dhidi ya Ufaransa.

Tume ya bunge la Ufaransa ya mwaka 1998 iliiondolea lawama Ufaransa kuhusu mauaji ya halaiki ya Rwanda lakini ilikiri kuwa makosa yalitendekea.