1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kikao cha kilele chaanza Copenhagen

7 Desemba 2009

Mkutano wa kilele wa mazingira unaanza rasmi hii leo mjini Copenhagen,Denmark.Viongozi wa mataifa na marais wanatarajiwa kukihudhuria kikao hicho kilicho na azma ya kuutafuta mktaba mpya utakaourithi ule wa Kyoto

https://p.dw.com/p/Kral
Nembo ya mkutano wa Copenhagen Cop15Picha: Cop15Copenhagen

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na athari za mabadiliko ya hali ya hewa Yvo de Boer amewatolea wito viongozi wa ulimwengu kuwa na msimamo wa pamoja wakati ambapo kikao cha kilele cha mazingira kinaanza rasmi hii leo.

De Boer alisema kuwa kuna haja ya kila nchi kutangaza bayana mchango wao ili mkutano huo uweze kufanikiwa.

UN Klimasekretär Yvo de Boer
Kiongozi UNFCCC, Yvo de BoerPicha: picture-alliance/ dpa

Lengo la kikao hicho cha siku kumi na mbili ni kufikia mkataba mpya utakaosaidia kuvipunguza viwango vya gesi za viwanda baada ya ule uliopo wa Kyoto kumaliza muda wake ifikapo mwaka 2012.