1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim aamuru uimarishwaji wa mazoezi ya kijeshi

Grace Kabogo
10 Machi 2023

Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameliamuru jeshi la nchi hiyo kuimarisha mazoezi ya "vita halisi".

https://p.dw.com/p/4OUOc
Nordkorea Kim Jong Un
Picha: Korean Central News Agency/Korea News Service/AP/picture alliance

Kwa mujibu wa shirika la habari la KCNA, wakati akikagua luteka ya kijeshi, Kim amewaambia wanajeshi wajiandae kwa operesheni mbili za kimkakati, ambazo kwanza ni kuzuia vita na pili kuchukua hatua katika vita.

Luteka hiyo inafanyika wakati ambapo Korea Kusini na Marekani zinajiandaa kuanza Jumatatu ijayo mazoezi makubwa ya pamoja ya kijeshi, katika kipindi cha miaka mitano.

Aidha, Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, ameapa kuimarisha luteka ya kijeshi na Marekani dhidi ya vitisho vya Korea Kaskazini vya kuanzisha mpango wa nyuklia