1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinara wa Umoja wa Mataifa aziomba pande mbili zinazohasimiana Kenya kumaliza tofauti zao kwa mazungumzo

1 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D164

NAIROBI:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa-Ban Ki-Moon yuko nchini Kenya kushiriki katika mazungumzo yenye nia ya kukomesha ghasia zilizoanza baada ya uchaguzi mkuu wa Disemba mwaka jana.Akizungumza katika mkutano na wajumbe wa rais Mwai Kibaki na wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga mjini Nairobi,ameziomba pande zote mbili kutatua mgogoro huo kupitia njia za mazungumzo.Hii inafuatia mkutano wake na rais Mwa Kibaki mjini Addis Ababa nchini Ethiopia siku ya alhamisi.Na leo Rais Kibaki,akiwa mjini addis Ababa, ameuambia mkutano wa viongozi wa mataifa yanayojumuishwa katika kundi la IGAD, kuwa mgogoro wa kuchaguliwa kwake,kuliko anzisha ghasia ni lazima utanzuliwe kupitia mahakama za Kenya.Hata hivyo jambo hilo linakataliwa na upande wa upinzani. Aidha ameulaumu upande huo,wa upinzani, kwa kuchochea ghasia ambazo zimesababisha watu zaidi ya 800 kuuawa katika nchi zamani iliokuwa inachukuliwa kama tulivu kuliko zingine katika kanda ya Afrika mashariki.

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa-Koffi Annan ameanza tena mazungumzo na pande zote mbili baada ya kuahirishwa kufuatia mauaji ya mbunge mwingine wa upande wa upinzani katika kipindi cha wiki moja.Polisi inayahusisha mauaji ya David Kimutai Too na suala la mapenzi.Aidha Polisi inasema kuwa imewauwa wandamanaji wanne kwa kuwapiga risasi ambao walikuwa wanapora mali na kuchoma moto nyumba katika mji wa Kericho.