1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Kampeni ya uchaguzi yaanza rasmi.

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD37

Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo , ikitapia kupata demokrasia baada ya miaka kadha ya udhalimu na vita ,usiku wa leo imeingia katika hatua ya mwisho katika utaratibu wa kumchagua kiongozi wake wa kwanza atakayechaguliwa katika uchaguzi huru katika muda wa zaidi ya miaka 40.

Baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi mwezi Julai mwaka huu kukumbwa na machafuko, siku 15 rasmi za kampeni zinaanza kwa ajili ya uchaguzi wa hapo Oktoba 29 ambapo kiongozi anayepigiwa upatu kupata ushindi Joseph Kabila anapambana na makamu wake wa rais na hasimu wake mkubwa Jean-Pierre Bemba .

Zaidi ya wapigakura milioni 25 watakuwa na haki ya kupiga kura kumchagua Kabila ama Bemba ambaye amepata asilimia 44.8 katika uchaguzi wa duru ya kwanza dhidi ya asilimia 20 za Bemba.

Uchaguzi wa serikali za mitaa utafuatia baada ya hapo.

Wakati huo huo treni iliyobeba tani 587 za chakula kwa ajili ya maeneo ya ndani ya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo imeondoka mjini Kinshasa jana Ijumaa katika operesheni kubwa kabisa kuwahi kutokea kwa miaka kadha, umesema mpango wa chakula wa umoja wa mataifa WFP.

Chakula hicho cha msaada kinalengwa kupelekwa kwa watu wa maeneo ya Bukama, Manono na Malemba-Nkulu, katika jimbo la Katanga.