1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Mwandishi habari auwawa

14 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBs0

Serge Maheshe mwandishi wa habari wa Congo anayefanya kazi na radio inayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa Radio Okapi amepigwa risasi na kuuwawa hapo jana katika mji wa mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wa Bukavu.

Maheshe mwenye umri wa miaka 31 aliuwawa wakati akiwa njiani mbele ya marafiki zake wawili.Walikuwa wakijiandaa kuingia kwenye gari lenye nembo za Umoja wa Mataifa mbele ya nyumba ya mtu mmoja waliokuwa wamtembelea.

Sababu ya kuuwawa kwake haikuweza kufahamika mara moja.