1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa.Wakongomani watakiwa kuwa watulivu ili kudumisha amani.

31 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxO

Umoja wa Mataifa umewataka wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kusubiri katika hali ya utulivu matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa Rais kati ya Rais anaemaliza muda wake Joseph Kabila na makamo wake Jean Piere Bemba.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUC imewatolea watetezi wote wawili, wafuasi wao na vyombo vya habari wito wa kujiepusha na kutoa tarakimu zisizokuwa na maana na za hatari, na kusubiri hadi matokeo yatakapotangazwa, November 19 ijayo.

Ufaransa, Ubelgiji na Umoja wa Ulaya wamezitaka pia pande hizo mbili ziheshimu uamuzi wa Umma, wakati matokeo hayo yatakapotangazwa.