1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyang'anyiro cha kuania madaraka

Hamidou, Oumilkher27 Oktoba 2008

Jinsi Seehofer alivyofanikiwa kutwaa madaraka ya CSU na Livni kushindwa kuunda serikali nchini Israel

https://p.dw.com/p/Fhe6
Mwenyekiti mpya wa chama cha CSU na waziri mkuu mteule wa jimbo la Bavaria Horst SeehoferPicha: AP



 Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi na mada tatu na zote zinahusu madaraka ya kisiasa;naiwe kuhusu uwezekano wa kuundwa serikali ya muungano kati ya SPD na walinzi wa mazingira katika jimbo la Hess,kushindwa juhudi za kuunda serikali nchini Israel au uongozi mpya katika jimbo la kusini la Bavaria.


Tuanzie kusini mwa Ujerumani ambako gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEUITUNG linatathmini mkutano mkuu wa dharura wa chama cha CSU kilichomchagua waziri wa kilimo wa serikali kuu ya Ujerumani Horst Seehofer kua mwenyekiti wake.Gazeti linaandika:


"Matokeo mabaya katika uchaguzi uliopita wa bunge jimboni humo,yamekiathiri vibaya sana chama CSU.Hata hivyo wana CSU wamegutuka kwa namna ambayo hawakuona muhali kumteuwa,Seehofer, mwanasiasa yule yule ambae mwaka mmoja tuu uliopita, hawakutaka awe mwenyekiti wao.Sio kwasababu wanampenda,hasha kwasababu hawana mwengine badala yake."


Lakini anaweza kweli Seehofer kukiokoa chama cha CSU? Linajiuliza gazeti la LAUSUTZER RUNDSCHAU la mjini Cottbus.


Kwa upande mmoja,mtu anaweza kusema anaweza.Seehofer ni bazi wa kweli,mcheshi,mwerevu na mwenye kipaji.Wabavaria wanampenda mtu kama huyo.Hata hivyo kuna zuka suala hapo,kuna wangapi kama yeye waliosalia katika chama cha CSU hivi sasa?Na hapao ndipo upande wa pili unapoanzia.Enzi za Beckstein na huber zimeonyesha jinsi CSU kinavyoweza kumeguka vipande vipande.Bila ya ufanisi ,hata CSU kinabainika kua chama cha kawaida tuu cha kisiasa."


Tukitoka kusini mwa Ujerumani tunaelelea Mashariki ya kati na hasa Israel ambako gazeti la  NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG linaandika kuhusu kushindwa juhudi za kuundwa serikali mpya.Gazeti linaendelea kuandika:


"Heka heka za kisiasa nchini Israel hazina dalili ya kumalizika.Kwanza ameng'atuka rais Katsav kutokana na kashfa ya mapenzi,,baadae akateleza waziri mkuu Ehud Olmert kutokana na kashfa ya rushwa na waziri wa mambo ya nchi za nje Tzipi Livni anashindwa kuunda serikali imara ya muungano.Sasa kuna kitisho cha kuitishwa uchaguzi mkuu kabla ya wakati na duru  zaidi za mazungumzo yasiyokua na tija.Ni hali inayotia uchungu hii.Hasa linapohusika suala la utaratibu wa amani pamoja na wapalastina.Kiongozi wa chama cha upinzani cha Likoud anashangiria.Na pindi makadirio ya awali ya maoni ya umma kuhusu chama chake yatathibitika uchaguzi ukiitishwa,basi matarajio ya kupatikana amani yatazidi kua finyu.